Grade 2 Kiswahili End Term 1
GRADE 2 END TERM ASSESSMENT – KISWAHILI
SECTION A
Jina: _______________________________________________
Shule: ______________________________________________
Gredi: ______________________________________________
Jinsia: Mvulana__________ Msichana_____________
Matumizi ya Mtaahini
Tumia vigezo na viwango vya kuthaminia vilivyopewa kwenye mwongozo wa mwalimu.
Kuzidisha Matarajio | Kufikisha Matarajio | Kukaribia Matarajio | Mbali Na Matarajio |
31-40 (80-100%) | 21-30(70-79%) | 11-20(60-69%) | 0-10(0-59%) |
ZOEZI LA KWANZA: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
SEHEMU YA KWANZA
Jitambulishe kwa kusema jina lako.
- Wanafunzi wenzako watatambulisha majina yao pia.
- Unasomea shule gani?
- Unasoma katika gredi gani?
Unapenda somo gani? (Mwanafunzi ajibu kisha apeane sababu)
- Mahojiano yawe na mazungumzo mafupi.
SEHEMU YA PILI
Msomee mwanafunzi kifungu kifuatacho mara mbili.
- Mwanafunzi asikilize vizuri kifungu.
“Leo ni siku ya furaha shuleni. Watoto wanacheza na kucheka. Mwalimu anaandika kwenye ubaoni. Kila mtoto ana kitabu chake. Leo watasoma hadithi nzuri. Baada ya masomo, watapumzika na kucheza nje.”
- Karibu na kwetu, kulikuwa na nini?
- Watoto wanafanya nini shuleni leo?
- Ni nini kitatokea baada ya masomo?
- Unafikiri watoto watapumzika vipi?
ZOEZI LA PILI: KUSOMA KWA SAUTI
Ukiwa tayari kuanza tathmini sema;
“Sasa naomba unisomee kifungu hiki kwa sauti.”
(maneno 50 kwa dakika 1)
“Mama yangu ni muuguzi. Kila siku anavaa koti jeupe la hospitalini. Anasaidia wagonjwa na kuwapa dawa. Marafiki zake wanamuita ‘Mama Afya.’ Wakati wa mapumziko, anapenda kupika na kutuletea vitafunio.”
ZOEZI LA TATU: MATUMIZI YA LUGHA
- Andika maneno haya vizuri
- a) Aju-
- b) Nija-
- Andika majina ya vifaa vya darasani.
- Tunga sentensi ukitumia neno “michezo.”
- Andika majibu sahihi ya salamu hizi
- Alamsiki?
- Hujambo?
- Andika majina ya nambari
- 1__________
- 2__________
- 3___________
ZOEZI LA NNE: KUANDIKA
Andika sentensi utakayosomewa na mwalimu.
- “Leo ni siku ya kipekee shuleni kwetu.”
- “Jioni, tutakwenda kucheza mpira na marafiki.”