Grade 1 Kiswahili End Term 1
GRADE 1
END TERM ASSESSMENT
TERM 1 2024
KISWAHILI SEHEMU YA A
Jina: _________________________________________________
Shule: ________________________________________________
Gredi: _________________________________________________
Jinsia: Mvulana __________ Msichana ___________
KWA MATUMIZI YA MTAHINI
VIWANGO VYA KUTHAMINI
Kuzidisha Matarajio | Kufikia matarajio | Kukaribia matarajio | Mbali na matarajio |
27-30 | 21-26 | 11-20 | 0-10 |
ZOEZI LA KWANZA: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
SEHEMU YA KWANZA
• Jitambulishe kwa kusema “Mimi ni mwanafunzi wa shule ya…”
• Muulize mwenzako jina lake.
a) Eleza kitu kimoja kuhusu shule yako. (mwenzako ajibu)
b) Unapenda somo gani zaidi shuleni? (mwenzako ajibu)
SEHEMU YA PILI
i) Msomlee mwenzako kifungu kifuatacho mara mbili.
ii) Mjulishe mwenzako kuwa atajibu maswali baada ya kusoma.
Leo asubuhi, nilienda shambani na familia yangu. Tulipanda mboga mbalimbali kama vile nyanya, pilipili, na maboga. Baada ya kazi nzito, tulirudi nyumbani na kufurahi pamoja.
a) Ni nini familia yenu iliyofanya leo asubuhi?
b) Mmevuna vitu gani shambani?
c) Unapenda shughuli gani za familia yako?
ZOEZI LA KUSOMA KWA SAUTI
Ukiwa tayari kuanza tathmini sema;
“Sasa naomba unisomee kifungu hiki kwa sauti.”
Leo tunajifunza umuhimu wa kufanya kazi pamoja na familia. Kupanda mboga ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano wetu na kujenga afya njema.
(maneno 40 kwa dakika 1)
KISWAHILI SEHEMU YA B
UFAHAMU WA KUSOMA, MATUMIZI YA LUGHA
1. Sehemu za mwili
Tunatumia mikono kulia chakula, kisha meno hutafuna. Chakula hicho huvunjwavunjwa na kuwa chepesi na rahisi. Mate hukitayarisha na kuipeleka tumboni kupitia kooni.
a) Tunatumia nini kutafuna chakula?
b) Chakula hupitia wapi ili kufika tumboni?
____________________________________________________________________________________ (2)
2. Mazingira
Mazingira ni pahali panapotuzunguka. Tunapaswa kutunza mazingira yetu. Tunaweza kufanya hivi kwa kupanda miti.
a) Mazingira ni nini?
_________________________________ (1)
b) Tunaweza kutunza mazingira yetu kwa kufanya nini?
_________________________________ (2)
3. Baba Yangu
Baba yangu ni fundi wa mbao. Pia anaweza kuitwa seremala. Yeye hutengeneza vitu kwa mbao kama meza, viti na kabati.
a) Baba hufanya kazi gani?
b) Fundi wa mbao huitwaje?
c) Taja vitu viwili ambavyo baba hutengeneza.
______________________________________________ (3)
4. Darasa la Maria
Maria yuko darasa la kwanza. Mwalimu wake anaitwa Bi. Neema. Bi. Neema akiingia darasani wanafunzi humuamkia “Shikamoo.” Darasa lao ni kubwa. Kwenye ukuta, kuna saa na chati. Darasa lina ubao mweusi.
a) Mwalimu wa Maria anaitwaje?
b) Taja vifaa viwili vya darasani
_____________________________________________________________________________________ (2)
5. Bendera Yetu
Bendera yetu ni ukumbusho wa historia yetu. Rangi nyeusi hutukumbusha mashujaa wetu waliopigania uhuru. Nyekundu hutukumbusha damu iliyomwagika. Ya kijani kibichi ni ukumbusho wa thamani ya nchi yetu na nyeupe ni ya amani.
a) Bendera yetu inatukumbusha nini?
b) Rangi ya kwanza, sehemu ya juu kwenye bendera ni gani?
c) Rangi nyekundu hutukumbusha nini?
_______________________________________________________________________________________ (3)
ZOEZI LA 2: MATUMIZI YA LUGHA
6. Jaza nafasi kwa herufi inayofaa
a) Kar _ t _ si
b) Da _ asa. (alama 2)
7. Jibu maswali sahihi
a) Ndizi _________________ zimeharibika. (zetu, langu)
b) Embe _________________ limeiva. (langu, zangu)
c) Viazi ______________ ni vikubwa. (chetu, vyetu) (alama 3)
8. Mama alipoenda sokoni alinunua machungwa 12. Andika nambari kwa maneno.
9. Siku ya kwanza ya wiki ni siku gani?
10. Andika sentensi hii kwa herufi kubwa
Alisoma kwa bidii
11. Andika jina la umbo hili
____________________________________________ (1)
ZOEZI LA 3: KUANDIKA
Mwalimu atasoma neno. Andika. (alama 4)
Andika sentensi tano kuhusu mwalimu wako.